Mdhamini wa ligi ya wilaya ya Iringa mjini Fredrick Mwakalebela.
Katibu
mkuu wa zamani wa shirikisho la soka nchini Tff Fredrik Mwakalebela ameomba kurefusha mkataba wake wa kudhamini ligi hiyo nakuahidi kuwa na
mikakati ya kuifanya ligi hiyo kuwa bora zaidi.
Akizungumza
katika hafla ya utoaji wa zawadi kwa timu zilizofanya vyema kwenye ligi hiyo
iliyomalizika miezi mitatu iliyopita mjini Iringa Mwakalebela amesema nia yake
ni kuona soka linachezwa na vijana kwakuwa michezo ni ajira.
Amesema
mpira wa miguu ni mmchezo unaopendwa zaidi dunia na unatoa ajira hivyo kama
wadau wataunga kwa pamoja kuzisaidia timu mbalimbali katika wilaya ya Iringa
huenda siku za usoni mkoa wa Iringa utaondokana na ukame wa kukosa timu ligi
kuu.
Aidha
mwakalebela amesema kama atafikia makubaliano na uongozi wa chama cha mpya
wilayani Iringa mjini IMDFA juu ya kumpa mkataba mpya atahakikisha anaboresha
maslahi ya timu shiriki kwenye ligi ya msimu ujao.
Mwakaleba
ameleza sababu kubwa ya kuomba udhamini zaidi kwenye ligi hiyo uongezwe kubwa zaidi ikiwa hali
duni ya kiuchumi ilivyo kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo ambapo mara nyingi
zimekuwa zikitembeza bakuli la kuomba misaada hata maji ya kunywa.
Katibu mkuu
huyo wa zamani wa Tff hakusita kutoa rai kwa wadau wenye uwezo wa kuendeleza
mchezo wa soka na michezo mingine wilayani humo na mkoa wa Iringa kwa ujumla
wafanye hivyo ili kuleta maendeleo zaidi.
Kwa upande
wake katibu mkuu wa chama cha mpira wilaya ya Iringa mjini Bakari kamtande
amesema wapo tayari kurefusha mkataba huo kwakuwa ligi yao ni yakwanza kupata mdhamini nchini lakini hiyo
itakuwa baada ya kuwekana sawa.
Kamtande
amechukua nafasi yake kwakuzipongeza timu zote 12 zilizoshiriki kwenye ligi ya
msimu huu kwakusema zilionyesha nidhamu ya hali ya juu tofauti na misimu
iliyopita kitu ambacho kimeonyesha ni ukomavu wa kifikra kwa viongozi wa timu
na wachezaji kwaujumla.
Pia katibu
huyo asiye na maneno mengi ametoa pongezi kwa mdhamini wao na kusema licha ya
kuchelezwesha zawadi amekamilisha makubaliano yaliyopo kwenye mkataba
walioandikishana nae.
Zawadi zilizotolewa na mdhamini wa ligi hiyo katibu mkuu wa zamani wa Tff
Fredrick Mwakalebela ni kama ifuatavyo.
1.Real moja
moja ....shilingi laki 5 jezi seti
1,mipira 5 na kikombe chenye thamani ya shilingi laki 6.
2.Mtwivila
city…shilingi laki 3,seti 1 ya jezi na mipira
3.
3.Mtwa fc…shilingi
laki 2,jezi seti 1 na mipira 2.
Nimu ya
nidham zima moto…shilingi laki 1, seti 1 ya jezi na mpira1.
Mfungaji
bora. Ni Endru chanungu maarufu kama Ambani wa mtwivila city amezawadiwa shilingi elfu 80.
katibu mkuu wa chama cha soka Iringa mjini Bakari Kamtande.
mwenyekiti wa chama cha soka Iringa mjini Ramadhani Mahano.
wawakilishi wa timu mbalimbali zilizoshiriki ligi ya wilaya msimu huu.
waandishi wa habari pia hawakuwa nyuma wakiongozwa na Denis Nyari wa Overcomers radio mwenye koti lenye rangi ya damu ya mzee.
Kombe la bingwa wa ligi hiyo timu ya Real Mojamoja
Mwakalebela kabla ya kugawa zawadi.
Jezi na mipira kabla ya kugawiwa kwa timu.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment