Pages

Ads 468x60px

Sunday, July 13, 2014

VAN GAAL:NATAKA UMOJA WA TIMU YA TAIFA YA UHOLANZI UHAMIE MANCHESTER UNITED.



                                   Louis Van Gaal.

Kocha mpya wa Manchester United Louis Van Gaal amesema wachezaji wa kikosi hicho  ni lazima wawe na umoja kama wa timu ya taifa ya Uholanzi ambaye ameiongoza kwenye fainali za kombe la dunia na kushika nafasi ya tatu mwaka huu.

Van Gaal ambaye anaanza rasmi kibarua chake kipya Old Trafford juma lijalo amesema anamatumaini makubwa kuwa kikosi cha Manchester United kitakuwa bora kama cha timu ya taifa ya Uholanzi.

Kocha huyo wa zamani wa Ajax, Barcelona na  Bayern Munich amesistiza kwamba  anaimani atafanya vizuri akiwa na Manchester United kitu amnachoamini kitawapa furaha mashabiki wa timu hiyo ambao msimu uliopita timu yao haikuwa na mwenendo mzuri chini ya David Moyes.

Wakati kukiwa na tetezi kuwa mshambuliaji wa Uholanzi na klabu ya Bayern Munich Arjen Roben kwamba anaweza kuhamia Manchester United  nyota huyo amesema hana mpango huo licha ya kuwa na mahusiano mazuri na Van Gaal.

                  Hapa Van Gaal akimpongeza nahodha wa Uholanzi Robin Van Persie.

                       Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment