Pages

Ads 468x60px

Thursday, July 17, 2014

LETENI PAUNDI MILIONI 70 KAMA MNAMTAKA RODRIGUEZ:MONACO.






                Jemes Rodriguez akiwa ndani ua uzi wa Monaco.

Vigogo wa soka nchini Ufaransa klabu ya Monaco imeuambia uongozi wa Real Madrid kuwa watoe kiasi cha Euro milioni 90 ambazo ni sawa na paundi milioni 70 kwaaajili ya kumsajili nyota wao Jemes Rodriguez.
Rodriguez  aliyeng’ara na kikosi cha timu ya taifa ya Colombia katika fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil alifunga magoli 6 na kuibuka mfungazi bora kwenye michuano hiyo ambayo ubingwa ulichukuliwa na Ujeruman.
Wakati uongozi wa Monaco ukiitaka Real Madrid kutoa dau hilo ili kunasa saini ya Mkolombia huyo mwenye umri wa miaka 23 chanzo kimoja cha habari barani Ulaya kimesema Manchester United inaweza kushindana na Real kwenye vita ya kumsaka kiungo huyo.
Real Madrid chini ya rais wake Florentino Perez inahaha kumsajili nyota huyo baada ya kuwepo kwa dalili za kuwauza nyota wake wawili Sami Khedira na Angel Di Maria ambao Arsenal na Manchester United zimekuwa zikiwafuatilia.
Rodriguez ambaye aliwahi kuicheza Fc Porto ya Ureno amefunga magoli 10 katika michezo 38 aliyocheza akiwa na Monaco  msimu uliopita na kuisaidia timu yake kufuzu kwenye Champions league msimu ujao.
Akiwa na kikosi cha Colombia kilichofuzu hatua ya robo fainali ya kombe la dunia mwaka huu nyota huyo mbali na kufunga magoli 6 nakuibuka mfungaji bora ali assist magoli 2,alipiga pass zilizokamilika 12 ikiwa ni uwiano wa asilimia 76 huku akipiga wastani wa mashuti 3.2 kwa kila mchezo aliocheza.



             Jemes Rodriguez akiwa katika jezi ya timu yake ya taifa ya Colombia.



 Jemes Rodriguez akibembelezwa na nyota wa Kibrazili Dani Alves na David Luiz baada ya Colombia kutolewa kwenye kombe la dunia hatua ya robo fainali ambapo walifungwa na Brazil magoli 2 kwa1.
 
                            Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment