Scolari.
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya
Brazil Luiz Felipe Scolari amewasilisha barua ya kujiuzulu nafasi hiyo kwa
uongozi wa shirikisho la soka nchini humo FA (CBF) baada ya kushindwa kumaliza
vyema fainali za kombe la dunia zilizomalizika usiku wa kuamkia leo na
Ujerumani kuwa bingwa.
Scolari mwenye umri wa miaka
65 amelazimika kufikia uamuzi huo baada ya kushindwa kutwaa ubingwa wa dunia
akiwa na kikosi hicho cha Brazil licha ya kufanya hivyo mwaka 2002 na katika
michezo 29 ameshinda michezo 19 pekee kwenye awamu ya pili akiwa anainoa
Brazil.
Pamoja na kuvuka hatua ya
makundi na kufika nusu fainali ya kombe la dunia mwaka huu Brazil ilikumbana na
kipigo cha michezo michezo miwili mfululizo kilichovunja rekodi ya taifa hilo
kupoteza mipambano miwili takribani miaka 39 iliyopita.
Kipigo hicho ambacho
kimeingia kwenye historia ya taifa hilo ni kile cha magoli 7 kwa 1 ambapo
ilikipokea kutoka kwa Ujerumani hatua ya nusu fainali kabla ya kufungwa na
Uholanzi magoli 3 kwa 0 kwenye pambano la kusaka mshindi wa tatu.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment