Pages

Ads 468x60px

Saturday, July 12, 2014

WATAKAOLETA VURUGU KESHO KATIKA JIJI LA RIO DE JENEIRO KUKIONA CHA MOTO.



       Askari wakiwa tayari kumkabili yeyote akatakaeleta fyoko mjini Rio De Jeneiro.

wakati pazia la michuano ya kombe la dunia likitaraji kufungwa kesho Ulinzi umeimarisha katika nchini ya Brazili ambayo kwa matra kadhaa kumekuwa kukiripotiwa kuwepo kwa maandamo.
Afisa mmoja mwandamizi nchini Brazil Jose Mariano Beltrame amesema kuwa mji wa Rio de Jeneiro unajiandaa kuweka usalama wa hali ya juu katika historia ya fainali ya kombe la dunia kati ya Argentina na Ujerumani hapo kesho.

Zaidi ya maafisa wa polisi wapatao  elfu ishirini na tano i,maafisa wa zima moto,pamoja na majeshi yatashirikishwa katika hatua hiyo.

Rais wa Brazil Dilma Roussef anatarajiwa kuhudhuria fainali hiyo katika uwanja wa Maracana akiandamana na marais wengine tisa akiwemo rais Vladmir Putin wa Urusi na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani.

Meli ishirini na tano zitakuwa zinapiga doria katika pwani ya mji huo.
Usalama vilevile utaimarishwa katika maeneo ambayo maelfu ya raia wa Argentina wamepiga kambi.

                    mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment