Pages

Ads 468x60px

Friday, July 25, 2014

ARTURO VIDAL AWATOLEA KWAPANI MAN UNITED.





                                  Arturo Vidal.

Ndoto za Manchester United kumsajili mchezaji wa Juventus na timu ya taifa ya Chile  Arturo Vidal, zimeota mbawa baada ya nyota  huyo kusema hanampango wa  kujiunga na timu hiyo.

Vidal ambaye amekuwa akihusishwa kuhamia old Traford kwa msimu huu wa usajili amesema kuwa anafuraha kuendelea kucheza  katika ligi kuu ya Italia hivyo.

Manchester united walianza kuonyesha nia ya kumwitaji mchezaji huyo akiwa na timu ya taifa ya Chile kwenye michuano ya kombe la dunia iliyomalizika hivi karibuni nchini Brazil baada ya kuonyesha kandanda safi.

Hata hivyo Vidal amesema kuwa atazungumza na kocha wa timu hiyo, Massimiliano Allegri kuhusiana na kutokuwa na mpango wowote wa kuondoka katika kikosi hicho na kwenda Manchester United.

                          Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment