Pages

Ads 468x60px

Friday, July 18, 2014

VICENTE DEL BOSQUE ASISTIZA KUTOACHIA NGAZI.





 Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Hispania Vicente Del Bosque.

Kocha mkuu wa mabingwa wa zamani wa kombe la dunia Hispania Vicente del Bosque ametangaza kuwa hana mpango wa kuachia nafasi yake  licha ya kutofanya vyema katika kombe la dunia mwaka huu.
Del Bosque mwenye umri wa miaka 63 amesema Hispania inaweza kufuta makosa yaliyojitokeza kwenye fainali za kombe la dunia na hatimae kurejea kwenye ubora waliokuwa nao hapo awali.

Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid amebainisha kwamba watahakikisha wanatetea ubingwa wa mataifa ya Ulaya mwakani kwakufanyia marekebisho dosari kadhaa zilizowagharimu na kupokonywa ubingwa wa dunia mwaka huu.

Hispania maarufu kama La Roja ilijikuta ikiaga fainali za kombe la dunia katika hatua ya makundi hali iliyosababisha taifa hilo kuporomoka katika ubora wa soka duniani hadi nafasi ya 8 kwatakwimu zilizotolewa jana na shirikisho la soka duniani Fifa.

                                  Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment