Pages

Ads 468x60px

Friday, July 11, 2014

NEYMAR AMWAGA CHOZI AKIZUNGUMZIA MADHAMBI ALIYOFANYIWA NA ZUNIGA.





Wakati mchezo wa kusaka mshindi wa tatu katika kombe la dunia  baina ya Brazil na Uholanzi ukitaraji kuchezwa kesho msambuliaji Neymar amejikuta akitokwa na machozi wakati akizungumzia  tukio la yeye kuumizwa na mlinzi wa Colombia Juan Zuniga.

Neymar ambaye alivunjika uti wa mgongo kwenye mchezo huo uliomalizika kwa Brazil kushinda magoli 2 kwa1 amesema tukio hilo halikuwa la kawaida  na kama  Zuniga angekuwa umbali wa sentimita mbili  kutoka alipokuwepo jeraha hilo lingemfanya apooze mwili.

Hata hivyo Neymar mwenye umri wa miaka 22 ameipa nafasi Argentina kunyakuwa kombe la dunia mwaka huu ikiwa na Leonel Messi kwakuwa mshindi huyo mara tano wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia ameshinda kila kitu hivyo huu ni wakati wake.

Neymar ambaye kesho atakuwa mtazamaji kwenye mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kati ya Brazil na Uholanzi hivi karibuni alionywa na daktari wa timu yake ya taifa kutolazimisha kucheza kabla hajapona vizuri na kinyume na hapo itakuwa hatari kubwa kwake.

 Hapa Neymar akisafirishwa kupelekwa Hospitali kwa ndege maalumu ya wagongwa.

 Jinsi tukio la kuumizwa kwa Neymar  lilivyokuwa,nyuma yake ni Zuniga mlinzi kisiki wa timu ya taifa ya Colombia.


                                 mkule.blogsport.com.

No comments:

Post a Comment