Pages

Ads 468x60px

Saturday, April 5, 2014

BAYER LEVERKUSEN YAMTUPIA VIRAGO KOCHA SAMI HYYPIA.



Uongozi wa timu ya soka ya Bayer Leverkusen ya Ujeruman umetangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha wao Sami Hyypia kufuatia timu hiyo kubugizwa magoli 2 kwa1 na Lowly Hamburg.

Uamuzi wa kumtupia virago kocha huyo unatokana na mwenendo mbaya wa timu ambapo katika michezo 14 imeshinda michezo 3 pekee pamoja na kipigo cha jana ijumaa dhidi ya Lowly Hamburg.

Matokeo ya jana yamezidi kuiweka pabaya timu hiyo katika kukata tiketi ya kushiriki ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao  na badala yake  nafasi ya kushiriki Uefa msimu ujao huenda ikaangukia kwa Wolfsburg  na Borussia Monchengladbach endapo timu hizo zitashinda michezo waliyonayo mwishoni mwa juma hili.

Hyypia ambae alianza kuinoa Leverkusen mwezi mei 2012 taarifa zimeeleza kuwa nafasi yake huenda ikachukuliwa na kocha wa timu ya vijana Sascha Lewandowski ambae atakuwa akimalizia michezo ya msimu huu wa Bundesiliga.

 Kiungo huyo wa zamani wa Liverpool mwenye umri wa miaka 40 mkataba wake wasasa ndani ya timu ya Leverkusen ulikuwa unamalizika katika msimu wa ligi mwaka 2015.
Posted by Yusuph Mkule. 

No comments:

Post a Comment