Pages

Ads 468x60px

Sunday, August 3, 2014

REAL MADRID YAMNYAKUA KIPA NO,1 WA TIMU YA TAIFA YA COSTA RICA.



                                      Keylor Navas.

Timu ya soka ya Real Madrid ya Hispania imekamilisha usajili wa mlindamlango Keylor Navas kutoka Levante kwa mkataba wa miaka sita ya kuwa Santiago Bernabeu.

Taarifa zilizothibitishwa na tovuti ya Real Madrid imeeleza kufikiwa kwa makubaliano baiana ya timu hizo mbili na sasa ni mchezaji halali wa mabingwa hao wa Ulaya kwa upande wa vilabu.

Navas  mwenye umri wa miaka  27 anataraji kutambulishwa rasmi katika timu ya Real Madrid kesho jumaane kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu mara baada ya kukamilisha vipimo vya afya.

Navas ambaye ni raia wa Costa Rica aliisadia nchi yake kufanya vyema kwenye fainali za kombe la dunia zilizomalizika mwezi uliopita nchini Brazil jambo lililovivutia vilabu mbalimbali duniani ikiwemo Real Madrid iliyomsajili.

                            Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment