Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 28, 2014

ALONSO KUFANYIWA VIPIMO LEO TAYARI KUJIUNGA NA BAYERN MUNICH.



                                       Xabi Alonso.

Mabingwa wa ligi kuu ya Ujerumani  Bayern Munich wametangaza kufikia makubaliano  na Real Madrid ya Hispania juu ya kumsajili  kiungo Xabi Alonso  na leo alhamisi mchezaji huyo anatarajiwa kuwasili Ujerumani kufanyiwa vipimo vya Afya.
Mabingwa hao wa Bundesiliga wamelazimika kusaka  mchezaji wa nafasi ya kiungo  baada ya kuumia kwa Javi Martinenz,Bastian Schweinsteiger na  Thiago Alcantara hivyo wanaamini Alonso mwenye umri wa miaka 32 anaweza kuwafaa kwa hivi sasa.
Taarifa za vilabu hivyo kufikia makubaliano ya kuuziana mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool zimethibitishwa na  mmoja wa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Bavarians Jan-Christian Dreesen kwenye mkutano wake na  waandishi wa habari.
Mjumbe huyo wa Bayern amethibitisha kwakuesema  Alonzo ambaye amecheza michezo zaidi ya 200 akiwa Santiago Bernabeu mara baada ya kufanyiwa vipimo leo mjini Munich  atasaini mkataba na kutua rasmi Allianz Arena.
  

                                  Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment