Kikosi cha mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Azam fc.
Mabingwa wa
ligi kuu ya soka Tanzania bara timu ya Azam fc ya jijini Daresalaam leo imeiaga
michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati maarufu kama Kagame baada ya
kutolewa kwa changamoto ya mikwaju ya Penalts 4 kwa 3 na Elmerekh ya Sudani.
Katika mchezo huo wa robo fainali
uliochezwa kwenye uwanja wa Nyamirambo Kigali Rwanda Azam fc ilitoka sare ya
kutofungana na Elmerekh ndipo changamoto
ya mikwaju ya matuta kutumika kumsaka mshindi.
Katika changamoto hiyo ya Matuta
Azam fc ilijikuta ikiambulia magoli 3 yaliyofungwa na wachezaji Agrey
Moris,Didier Kavumbagu na Ereasto Nyoni huku mkwaju wa beki wa kupanda na
kushuka Shomari Kapombe ukigonga mtambaa panya kabla ya Leonel Saint- Preux shuti
lake kudakwa na mlindamlango wa Elmerekh.
Mlinda mlango wa Azam fc Mwadini
Ally Mwadin alifanikiwa kupangua mkwaju mmoja wa Penalti kisha kufungwa mikwaju
minne kati ya mitano iliyopigwa na wachezaji wa Elmerekh.
Wakati Azam fc ikijiandaa kurejea
nyumbani baada ya kuiga michuano hiyo ya mwaka huu ambapo mabingwa hao wa ligi
kuu ya soka Tanzania bara walipata bahati kufuatia Yanga kuenguliwa na CECAFA
Elmerekh imeungana na Polisi pamoja na APR zote za nchini Rwanda kutinga nusu
fainali.
Robo fainali ya pili hii leo ni
baina ya KCCA ya Uganda na Atlabara juba ya Sudani kusini.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment