Sunday, August 24, 2014
UWANJA WA TIMU YA SHAKTAR DONETSK WALIPULIWA NA MABOMU NCHINI UKRAIN.
Uwanja wa Donbass Arena baada ya kulipuliwa na mabomu.
Ghasia nchini Ukrain zimeendelea kusababisha maafa hata kwenye miundombinu ya michezo baada ya mabomu mawili kuharibu uwanja wa Donbass Arena unaomilikiwa na klabu ya Shaktar Donetsk inayoshiriki ligi kuu ya huko.
Mabomu hayo yaliyolipuka jana licha ya kutojeruhi mtu yeyote yameharibu vifaa vya mawasiliano vilivyoko kwenye uwanja huo ambao ulitumika katika nusu fainali ya mataifa ya Ulaya mwaka 2012 baina ya Hispania na Ureno.
Uwanja huo pia ulitumiwa na Shaktar Donetsk walipokuwa wanacheza na Manchester United mwezi wa kumi mwaka jana kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya ambapo timu hizo zilitoka sare ya kufungana goli 1 kwa 1.
Tayari timu ya Shaktar Donetsk imeshahama kwenye mji wa Donetsk yalipo makazi yao na kuhamia mji wa Lviv ambapo michezo yao ya ligi ikiwemo ile ya klabu bingwa Ulaya itachezwa huko kutokana na machafuko yanayoendelea Ukrain.
Uwanja wa Donbass Arena unavyonekana dani kabla ya kulipuliwa na mabomu
Uwanja wa Donbass Arena unavyonekana kwa nje kabla ya kulipuliwa na mabomu
Mkule.blogsport.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment