Pages

Ads 468x60px

Friday, August 15, 2014

LIPULI FC YAKAMILISHA USAJILI WAKE,KUINGIA KAMBINI AUGOST 29.






Timu ya soka ya Lipuli fc ya mkoani Iringa imekamilisha usajili wake tayari kwakujiandaa na msimu mpya wa ligi daraja la kwanza Tanzania bara unaotaraji kuanza baadae mwaka huu kwakutanisha vilabu mbalimbali.

Mwenyekiti wa muda wa timu hiyo Reanatus Kalinga amesema  usajili wamesha uwasilisha katika shirikisho la soka nchini Tff  na kilochosalia ni maandalizi ya mwishomwisho kuelea kwenye kambi inayotaraji kuanza Augost 29.

Kalinga amesema katika usajili wao msimu huu hawajasajili wachezaji wenye majina makubwa kuwakuwa msimu uliopita jambo hilo liliwadharimu kwani wengi wao hawakucheza soka kwa kiwango kilochotarajiwa na wengi.

Amesema msimu huu wa usajili wamefanya usajili kwa kuzingatia uwezo na sio majina hivyo mashabiki wa timu hiyo na dau wote wa soka mkoani Iringa kujiandaa kuiona Lipuli ikiwa kwenye muonekano wa tofauti na msimu uliopita.

Amebainisha kuwa lengo kuu kwao ni kuhakikisha timu ya Lipuli inapanda daraja baada ya kusota kwa muda murefu bila mafanikio tangu ishuke daraja zaidi ya miaka 10 iliyopita.

Amesema imani ya kupanda ligi kuu inatokana na usajili mzuri walioufanya na hilo hakina shaka kwamba ile kiu ya mashabiki wa soka mkoani humo kutoona ligi kuu itakatwa na wao.


Kalinga amehimiza mshikamano miongoni mwa wanachama na mashabiki wote wa soka katika mkoa huo katika kuwaunga mkoano kwani kufanya hivyo kutasaidia kufikia mafanikio makubwa waliyojiwekea.

Amesema kambi ya Lipuli fc itaanzia katika chuo cha ualimu Kleruu kilichopo mjini Iringa na mara baada ya wachezaji wote kuwasili timu hiyo itaingia mafichoni kujifua zaidi na msimu mpya wa ligi daraja la kwanza Tanzania bara (FDL)2014/2015.

                                     Mkule.blogsport.com




No comments:

Post a Comment