Pages

Ads 468x60px

Monday, August 11, 2014

KINARA WA MABAO KOMBE LA DUNIA ASTAAFU SOKA LA KIMATAIFA.





   Miroslav Klose akiwa  na kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ujeruman Joachim Low.

Mshambuliaji wa Lazio ya Italia na timu ya taifa ya Ujeruman Miroslav Klose ametangaza rasmi kustaafu kitumikia timu yake ya taifa  akiwa na umri wa miaka 36.
Klose ambaye katika fainali za kombe la dunia mwaka huu ameisaidia Ujeruman kutwaa ubingwa kwenye fainali zilizofanyika nchini Brazil amestaafu akiwa anashikilia rekodi ya kuwa  mfungaji wa muda wote wa fainali hizo kwakufikisha magoli 16.
Mkongwe huyo ambaye hatosahaulika kwenye soka la kimataifa kutokana na uhodari wake aliokuwa nao wa kufunga magoli ya kishwa kwenye fainali za mwaka huu alifanikiwa kufunga magoli  mawili katika michezo mitano aliyocheza.
Akizungumzia uamuzi wake wa kustaafu Klose amesema anashukuru kutimiza ndoto ya kutwaa kombe la dunia katika maisha yake ya soka na hakuna njia nyingine ya kustafu soka kama sasa ilikuwapisha vijana.
Nyota huyo amesema katika maisha yake ya soka kuitumikia timu ya taifa lilikuwa jambo la kwanza  na alikuwa hafikirii kuweka rekodi bali kuchezwa kwa moyo wake wote kwenye timu ya taifa na kazi yake ilikuwa kufunga magoli.

          Miroslav Klose akiwa ameshikilia kombe la dunia mwezi jana nchini Brazil

Klose alicheza mchezo wake wa kwanza kwenye timu ya taifa ya Ujerumani mwezi wa 3 mwaka 2001 ambapo Ujerumani iliifunga Albania magoli 2 kwa 1 na alifunga goli la ushindi dakika 19 klaby ya pambano hilo kumalizika.
Hadi na tundika daluga mkongwe huyo amecheza michezo 137 akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Ujeruman akiwa nyuma ya mkongwe Lothar Matthaus aliyecheza michezo 150.
                              Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment