Pages

Ads 468x60px

Monday, August 11, 2014

WENGER KUONGEZA BEKI WA KATI KUZIBA NAFAI YA VERMAELEN.



                                        Arsene Wenger.

Kocha mkuu wa timu ya Arsenal mfaransa Arsene Wenger amesema anampango ya kutafuta mlinzi wakati atakaechukua nafasi ya Thomas Vermaelen ambaye amesajiliwa na vigogo vya soka nchini Hispania klabu ya Fc Barcelona.
Licha ya uwezo mzuri ulioonyeshwa na chipkizi Calum Chambers jana jumapili kwenye mchezo wa ngao ya jamii ambapo Arsenal ilifanikiwa kushinda magoli 3 kwa 0 ddhidi ya Manchester City kocha Arsene Wenger amesema atatafuta mbadala wa Vermaelen.
Japo kocha huyo amekiri kuwa sio jambo rahisi kupata mlinzi mzuri kwa haraka lakini kama itawezekana kufanya usajili kipindi hiki atahakikisha nafanya hivyo licha ya kuridhishwa na uwezo wa Chambers hapo jana.
Arsenal ambaye imeonyesha uwezo mzuri hapo jana kwakuwafunga mabingwa wa lighi kuu ya England kocha mkuu ambaye amedumu na kikosi hicho muda mrefu amesema kwasasa wachezaji wote wapo tayari kwaajili ya msimu mpya unaoanza mwishoni mwa juma hili.

                       Mkule.blogsports.com

No comments:

Post a Comment