Pages

Ads 468x60px

Friday, August 8, 2014

ETHIOPIA YAWASILI BRAZIL KWA KAMBI YA WIKI MBILI KUJIANDAA NA HATUA YA MAKUNDI KUFUZU AFCON 2015.




 
                Kikosi cha timu ya taifa ya Ethiopia.

Timu ya taifa ya Ethiopia imewasili nchini Brazil tayari kwaajili ya kuweka kambi kwa wiki mbili kujiandaa na hatua ya makundi  kusaka tiketi ya kuchezea fainali za Afrika mwakani ambazo zitafanyika Morocco kuanzia mwezi wa  kwanza.
Ikiwa nchini Brazil Ethiopia itacheza michezo mitano ya kirafiki na vilabu mbalimbali vya nchini humo ikiwemo AC Anapolina Club Do Remo kwenye uwanja wa  Arena Baenao Gama, pia watacheza na Brasiliense kwenye uwanja wa  Boca do Jacare.
Pambano lao la mwisho litakuwa dhidi ya timu ya  Itubiara kwenye uwanja wa  seater JK stadium.
Wakiwa nchini Brazil watakuwa katika hoteli ya San Peter na watakuwa wakifanya mazoezi kwenye mmoja ya vituo ambavyo vilitumiwa na timu ya taifa ya Brazil wakati wa fainali za kombe la dunia zilizomalizika mwezi uliopita na Ujerumani kuibuka bingwa.
Kikiwa chini ya kocha mkuu Mariano Barreto akisaidiwa na Daniel Tsehai madaktari  timu  Dr. Terefe Tafa,na  Physio Behailu Abera.


                   Kikosi cha timu ya taifa ya Ethiopia kilichoshiriki fainali za AFCON 2013 Afrika ya kusini.

Miongoni mwa wachezaji waliowasili nchini Brazil ni pamoja na Jemal Tassew, Sesay Bancha, Ephrem Ashamo, Mesud Mohammed, Shemeles Tegegn, Andaregachew Yelake, Thok James, Abebaw Butako, Behanu Bogale, Mintesinot Adane, Akilu Ayanaw na  Dawa Hottesa.

Kikosi kizima cha Ethiopia kitakachukuwa nchini Brazil ni pamoja na  Minyahile Teshome, Asrat Megersa, Salahdin Bergecho, Shemelis Bekele, Fikru Teffera, Natnael Zelleke, Fitsum Gebremariam, Behailu Assefa, Adane Girma, Gathoch Panom, Fasil Tekalegne,kocha wa makipa   Haileselaise Georgis na kiongozi wa timu ndgYosef Tesfaye.
Katika kusaka tiketi ya kucheza fainali za AFCON mwanaini Ethiopia ipo kundi mmoja na Malawi,Mali na Algeria.

                                        Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment