Pages

Ads 468x60px

Monday, August 18, 2014

KIPIGO CHA SWANSEA CITY CHAMPELEKA VAN GAAL SOKONI ANASA BEKI MPYA.




                                            Marcos Rojo.

Klabu ya Manchester United ya England imefikia makubaliano ya kumsajili mlinzi wa timu ya Sporting Lisbon ya Ureno Marcos Rojo kwa ada ya Euro milioni 20 sambamba na kumtoa kwa mkopo wa muda mrefu mchezaji Luis Nani.
 Rojo mwenye umri wa miaka 24 anatarajiwa kuwasili Old Traford baada ya makubaliano hayo kufikiwa na klabu zote mbili na raia huyo wa Argentina atarudi Ureno kwaajili ya kuwaaga wachezaji wenzake wa Sporting na mashabikiwa timu hiyo.
Kocha wa Man  United Louis Van Gaal ametoa sababu ya kusajili mlinzi huyo  kwakusema anauwezo mkubwa wa kucheza mfumo anayoutumia  baada ya  kufungwa na Swansea City magoli 2 kwa 1 katika ligi kuu ya England siku ya jumamosi.



Katika mauzo ya mchezaji huyo Sporting itailipa timu ya Spartak Moscow Euro milioni 5 ambayo aliichezea Rojo na asilimia 75 itaenda kwa taasisi ya Doyen Sport ambayo inamiliki hati za kiuchumi za mchezaji hivyo Sporting haitaambulia chochote.

                             Mkule.blogsport.com.

No comments:

Post a Comment