Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 28, 2014

CR7 MCHEZAJI BORA WA ULAYA ASEMA TUZO ZOTE KUZIWEKA KWENYE MAKUMBUSHO YAKE.

                Cristiano Ronaldo akipokea tuzo yake leo kutoka kwa raisi wa Uefa Michel Platin.

Mshambuliaji hatari wa Real Madrid ya Hispania na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ulaya na kutwaa tuzo mbele ya mshambulizi wa Bayern Munich na mlindamlango wa mabingwa hao wa Bundesiliga Manuel Neur.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 29 amefunga magoli 17 katika msimu uliopita wa michuano ya klabu bingwa Ulaya na kuisaidia timu yake ya Real Madrid kunyakuwa taji hilo baada ya kuifunga Atletico madrid kwenye pambano la  fainali pambano lililochezwa jijini Lisbon Ureno.
                      CR7 akibusu tuzo yake ya mchezaji bora wa Ulaya 2013/2014.

Akizungumza mara baada ya kushinda tuzo hiyo ya mchezaji bora wa Ulaya msimu uliopita Ronaldo amesema  anajisikia furaha nakuwashukuru wachezaji wenzake wa Real kwakusema bila wao asingeibuka mshindi wa tuzo hiyo iliyokuwa ikiwaniwa na wachezaji wengi.

Ronaldo aliyejiunga na Real Madrid mwaka 2009 akitokea Manchester United amesema ni vigumu sana mchezaji mmoja kushinda tuzo hiyo bali ushirikiano mziuri alioupata kutoka kwa wenzake ndiyo chanzo cha mafanikio aliyoyapata bila kuwasahau viongozi wa timu hiyo na mashabiki wake wote duniani.

          Wakwanza kulia Manuel Neuer,C.Ronald katiakati na wamwisho kushoto Arjen Robben.

Ronaldo amewashinda Neuer na Roben baada ya kupata kura 54 kutoka kwa waandishi wa habari.


WASHINDI WALIOPITA  WA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA ULAYA.

2010-11 Lionel Messi (Barcelona)
2011-12 Andres Iniesta (Barcelona)
2012-13 Franck Ribery (Bayern Munich)

Mlindamlango Manuel Neuer  mwenye umri wa miaka, 28 aliisaidia Ujerumani kutwaa kombe la dunia wakati Robben mwenye umri wa miaka 30 alifunga magoli 21 akiwa na Bayern Munich  na matau kwa timu yake ta taifa ya Uholanzi  yaliyosaidia kuifikisha nchi hiyo hatua ya nusu fainali ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
 Katika orodha ya wachezaji 10 waliokuwa wanashindania tuzo hiyo wengine ni: 4 Thomas Muller (Bayern Munich, Germany); 5= Philipp Lahm (Bayern Munich, Germany), 5= Lionel Messi (Barcelona, Argentina); 7 James Rodriguez (Monaco/Real Madrid, Colombia); 8 Luis Suarez (Liverpool/Barcelona, Uruguay); 9 Angel Di Maria (Real Madrid/Manchester United, Argentina); 10 Diego Costa (Atletico Madrid/Chelsea, Spain).

YAFUATAYO  NI MAKUNDI YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE 2014/2015.




Group A: Club Atlético de Madrid, Juventus, Olympiacos FC, Malmö FF 
Group B: Real Madrid CF, FC Basel 1893, Liverpool FC, PFC Ludogorets Razgrad
Group C: SL Benfica, FC Zenit, Bayer 04 Leverkusen, AS Monaco FC
Group D: Arsenal FC, Borussia Dortmund, Galatasaray AŞ, RSC Anderlecht
Group E: FC Bayern München, Manchester City FC, PFC CSKA Moskva, AS Roma
Group F: FC Barcelona, Paris Saint-Germain, AFC Ajax, APOEL FC
Group G: Chelsea FC, FC Schalke 04, Sporting Clube de Portugal,
NK Maribor
Group H: FC Porto, FC Shakhtar Donetsk, Athletic Club, FC BATE Borisov.


Michezo ya awali itaanza kuchezwa tarehe 16-17/09/2014.
 
Matchday two 30/09–01/10/14
Matchday three 21–22/10/14
Matchday four 04–05/11/14
Matchday five 25–26/11/14
Matchday six 09–10/12/14.


                                        Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment