Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 20, 2014

DUNGA AWAACHA MARCELO,JO,DANTE,DANI ALVES NA JULIO CESAR KATIKA KIKOSI CHA BRAZIL.


                       Dunga,kocha wa sasa wa timu ya taifa ya Brazil.

Kocha mpya wa timu ya Taifa ya Brazil Dunga ametangaza kikosi chake cha kwanza tangu ateuliwe kuchukua nafasi ya Luis Felipe Scolar mwezi uliopita aliyeacha kazi baada ya kushindwa kutwaa ubingwa wa dunia kwenye fainali za mwaka huu zilizofanyika nchini Brazi na Ujerumani kuibuka machampioni kwa kuifunga Argentina goli 1 kwa 0.

Katika kikosi hicho kitakachocheza michezo ya kirafiki na Colombia pamoja na Ecudor Dunga amewaacha baadhi ya wachezaji waliokuwepo kwenye timu ya taifa ya Brazil ilioadhiriwa na Ujerumani kwakufungwa magoli 7 kwa 1 kwenye hatua ya nusu fainali ya kombe la dunia mwaka huu.
                     Nyota wa Liverpool,Coutinho ndani ya kikosi cha Dunga

walioachwa ni Julio Cesar, Victor, Dani Alves, Marcelo, Dante, Maxwell, Henrique, Paulinho, Hernanes, Bernard, Jo.

Kikosi kizima cha Brazil hivi sasa hikihapa Neymar akijumuishwa ndani.
                               Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment