Mkongwe wa Real Madrid Luis Figo akiwatoka walinzi wa Tanzania Eleven jioni ya leo kwenye uwanja wa taifa jijini Daresalaam.
Timu ya soka
ya Tanzania Eleven inayojumuisha wakongwe wa Tanzania waliowahi kung’ara na
timu mbalimbali nchini pamoja na timu ya taifa leo imechezea kichapo cha magoli
3 kwa 1 kutoka kwa wakongwe wa Real
Madrid ya Hispania kwenye pambano la kirafiki
liliochezwa uwanja wa taifa jijini Daresalaam.
Katika
pambano hilo lilohudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania mh.daktari Jakaya Kikwete hadi mapumziko timu hizo
zilikuwa zimefungana goli 1 kwa 1.
Kipindi cha
pili pamoja na mabadiliko kadha a yaliyokuwa yakifanywa na kocha mkuu wa timu
ya Tanzania Eleven Charles Bonifas Mkwasa na msaidizi wake Jamhuri Kiwelu Julio
kikosi hicho kilishindwa kufua dafu mbele ya wakongwe wa Real Madrid waliokuwa
wakiongozwa vyema na Luis Figo.
Katika pambano
hilo magoli yote ya wakongwe wa Real Madrid yalitiwa kambani na mchezaji De
la Red kunako dakika za 10,81 na 88 goli
la dkk 81 lilikuwa la mkwaju wa penalt baada ya mfungaji huo kuchezwa madhambi
ndani ya maguu 18 ya mtu mzima.
Pao pekee la Tanzania Eleven lilipatikana dkk ya 45
ambapo mkongwe wa Real Madrid Roberto Rojas alijifunga katika harakati za
kuokoa mpira wa kona uliochongwa na nahodha wa zamani wa Taifa Stars na kocha
wa sasa wa mtibwa sukari Meck Mexime.
Hadi dakika 90 zinamalizika wakongwe wa Real Madrid 3
tanzania Eleven goli 1.
Miongoni mwa nyota wa Tanzania waliocheza hii leo ni
..Mohamed Mwameja amabye baadae nafasi yake ilichukuliwa na Piter Manyika,Meck
Mexime,Kalimangonga Ongala,Habibu Kondo,Shadrack Nsajigwa, Shabn Ramadhani ,Madaraka Suleiman na Athman China.
Baada ya pambano hilo usimu huu wachezaji wote wanataraji
kula shakula cha pamoja na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh.Jakaya Kikwete
Ikulu jiji Daresalaam.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment