Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 20, 2014

JULIO CESAR ATUA BENFICA NA KUMWAGA WINO WA MIAKA MIWILI.




                                       Mlindamlango mpya wa Benfica Julio Cesar.

Timu ya Benfica ya nchini Ureno imethibitisha kumsajili mlinda mlango Julio Cesar kwa uhamisho huru baada ya klabu ya QPR kukatisha mkataba wake wa miaka miwili uliokuwa umesalia kwa makubaliano ya pamoja.
Nyota huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Brzail amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Benfica  inaotumia uwanja wa Estadio da Luz na atakuwa chaguo la kwanza baada ya kuondoka kwa mlindamlango Jan Oblak aliyejiunga na Atletico Madrid.
Cesar ambaye  alijiunga na QPR msimu wa 2012  ametumia nusu ya msimu uliopita akicheza kwa mkopo katika timu ya Toronto ya Marekani kabla ya kuitumikia timu ya taifa ya Brazil kwenye fainali za mwaka huu za kombe la dunia.
 Raia huyo wa Brazil aliyecheza michezo 27 akiwa na QPR  timu ya Benfica ni klabu yake ya nne kuichezea katika hitoria yake ya soka baada ya kuzitumikia  Flamengo na Inter Milan ya Italia.

                            Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment