Pages

Ads 468x60px

Tuesday, August 19, 2014

APR NA POLISI ZATINGA NUSU FAINALI YA MICHUANO YA KAGAME.



           Wawaklishi wa Tanzania bara katika michuano ya Kagame mwaka huu timu ya Azam fc.

Timu za Polisi ya Rwanda na APR zote za nchini Rwanda zimefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati maarufu kama Kagame baada ya kuibuka na ushindi kwenye michezo yao ya robo fainali.

Katika michezo iliyochezwa jioni ya leo mjini Kigali Rwanda timu ya maafande wa Polisi wa nchini humo wameingia nusu fainali baada ya kuwafunga kwa matuta timu ya Atletico ya Burundi baada ya kutofungana katika muda wa dakika 90.
katika changamoto hiyo ya mikwaju ya penalti Polisi iliikwamisha kimiani penalti 9 wakati wapinzani wao timu ya Atletico wakipata penalti 8.
Nayo timu ya APR yenyewe imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuiondosha mashindanoni timu ya Rayo Sports ya Rwanda kwa changamoto ya mikwaju 4 kwa 3.
timu hizo zilifikia kupigiana matuta kufuatia kwenda sare ya kufungana magoli 2 kwa 2 katika muda wa dakika 90.

Kesho michuano hiyo itaendelea ambapo Azam fc ya Tanzania bara itakuwa uwanjani kuikabili El Merreikh ya Sudani wakati timu ya Atlabara Juba ya Sudani kusini itakuwa ikivaana na KCCA ya nchini Uganda.

                                      Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment