Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 14, 2014

COPA COCA COLA NGAZI YA MKOA WA IRINGA YAANZA,TATIZO LA VIJEBA LAENDELEA KUWEPO.



      Kikosi cha timu ya Copa coca cola wilaya ya ringa manispaa kilichocheza jana na Kilolo.

Wakati mashindano ya Copacoca cola ngazi ya mkoa wa Iringa yakianza changamoto ya umri imeendelea kujitokeza licha ya wasimamizi wa mashindano hayo kuelewa umri wa wachezaji wanaotakiwa kushiriki.

Blog hii jana ilitembelea katika uwanja wa Samora ambapo kulichezwa pambano baina ya Iringa manispaa na Kilolo na kushuhudia utaratibu mbovu uliotumika kuruhusu mchezo kuchezwa bila kukaguliwa kwa vyeti vya kuzaliwa vya wachezaji wa pande zote.

Kufuatia hali hiyo katibu mkuu wa chama cha mpira wilaya ya Kilolo Editon Mbilinyi  ameonyesha kukerwa na utaratibu huo huku akilalamikia wapinzani wao kuchezesha vijeba.

Mbilinyi pia aliuponda mfumo uliotumika mwaka huu kuunda timu za wilaya kwakuhusisha mabonanza ambayo amesema hayasaidii kupata wachezaji wazuri kwakuwa yanafanyika kwa siku mmoja tuu.

Alisema kuwa endapo mtindo huo utaendelea kutumiwa na Tff badala ya ule wa zamani wakuanzia ngazi ya mashule ambapo mashindano maalumu yalikuwa yana fanyika kupata timu nzuri za wilaya hadi mkoa  taaswira halisi ya michuano hiyo  itapotea.

Alisema katika pambano hilo la jana manispaa ya Iringa ilitumia wachezaji vijeba badala ya kutumia wachezaji husika wanaotakiwa ambao ni wale wenye umri usizidi miaka  15.

Kwa upande wake katibu mkuu msaidizi wa chama cha soka  mkoa wa Iringa John Ambwene alisema walilazimika kuruhusu michezo ya mwazo iliyoanza jana kuchezwa bila kukagua umri wa wachezaji kutokana na kukurubushwa kufanya mashindano hayo.

Hatahivyo Ambwene alisema michezo iliosalia yote itafanyika kwa wachezaji kukaguliwa umri wao kupitia vyeti vya kuzaliwa na mchezaji yeyote atakaebainika kuwa na umri mkubwa  ataondolewa mara moja.

Aidha katibu huyo msaidizi alisema kuwa haya yote yanatokana na Tff kuwaburusha wanachama wake  kwenye maandalizi ya mashindano ya Copa Coca Cola mwaka huu  huku alilalamikia wadhamini kutowasilisha hela za kuandalia mashindano hayo.

Katika michezo ya jana timu ya Manispaa ya Iringa lifanikiwa kuifunga timu ya wilaya ya Kilolo magoli 5 kwa 1 huku kikosi cha Manispaa ya Iringa kikionekana kuwa na wachezaji wenye umri wa zaidi ya miaka 15.

Katika mchezo mwengine uliochezwa wilaya ya Iringa vijijini timu ya wilaya ya Mufindi ilifungwa goli 1 kwa 0 na Iringa vijijini pambano lilochezwa kwenye uwanja wa shule ya msingi Tangangozi.


         Kikosi cha timu ya Copa coca cola wilaya ya Kilolo kilichocheza jana na Iringa manispaa.



                 miongoni mwa wachezaji wa Copacoca cola wa manispaa ya Iringa.

Kwamujibu wa katibu msaidizi wa chama cha soka mkoa wa Iringa John Ambwene mashindano hayo ya Copacoacola ngazi ya mkoa yataendelea mwishoni mwa wiki hii katika uwanja washule ya msingi Tanangozi uliyopo Iringa vijijini siku ya jumamosi nakufikia tamati jumapili kwenye uwanja huohuo.

Mara baada ya hapo timu ya mkoa wa Iringa ya Copa Coca cola itatangazwa ikiwa chini ya kocha mkuu Dudu Harou akisaidiwa na Fidelis Kalinga tayari kwamashindano ya taifa.

                                    Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment