Pages

Ads 468x60px

Sunday, August 31, 2014

SUPER MARIO BALOTELLI ATEMWA KATIKA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA ITALIA.



                    Kocha wa timu ya taifa ya Italia Antonio Conte.

Kocha mpya wa timu ya taifa ya Italia Antonio Conte ametangaza kikosi chake cha kwanza tangu apewe jukumu la kukifundisha kikosi hicho  huku kwenye orodha hiyo jina la mshambuliaji mpya wa Liverpool Mario Baloteli likikosekana.

Kikosi hicho ambacho ni chakwanza tangu Conte achukue nafasi ya Cesare Prandelli aliyejiuzulu baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Uruguay kwenye fainali za kombe la dunia mwaka huu zilizofanyika nchini Brazil.

Uteuzi wa kikosi hicho ni kwaajili ya mchezo wa kirafiki na Uholanzi utakaochezwa septemba 4 mwaka huu kabla ya kuikabili Norway siku tano baadae kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Ulaya mwaka 2016.

Licha ya Balotelli kuachwa kocha Antonio Conte amewaita mlinda mlango mkongwe Jiji Buffon na wachezaji wengine kama , Giorgio Chiellini, Leonardo Bonucci, Daniele De Rossi na Claudio Marchisio  wote wamejumuishwa pamoja na  Ciro Immobile, Simone Zaza na Sebastian Giovinco.

Kikosi kamili cha Italia hiki hapa:-


Goalkeepers: Gianluigi Buffon (Juventus), Daniele Padelli (Torino), Mattia Perin (Genoa), Salvatore Sirigu (Paris Saint Germain);

Defenders: Davide Astori (Roma), Leonardo Bonucci (Juventus), Giorgio Chiellini (Juventus), Gabriel Paletta (Parma), Andrea Ranocchia (Inter);

Midfielders: Antonio Candreva (Lazio), Matteo Darmian (Torino), Daniele De Rossi (Roma), Mattia De Sciglio (Milan), Alessandro Florenzi (Roma), Emanuele Giaccherini (Sunderland), Christian Maggio (Napoli), Claudio Marchisio (Juventus), Marco Parolo (Lazio), Manuel Pasqual (Fiorentina), Andrea Poli (Milan), Marco Verratti (Paris Saint Germain);

Attackers: Mattia Destro (Roma), Stephan El Shaarawy (Milan), Sebastian Giovinco (Juventus), Ciro Immobile (Borussia Dortmund), Pablo Osvaldo (Inter), Simone Zaza (Sassuolo).



                                   Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment