Pages

Ads 468x60px

Tuesday, August 19, 2014

MOURINHO:NAHITAJI CECH AENDELEE KUBAKI DARAJANI.




                                             Petr Cech.

Kocha wa timu ya Chelsea Jose Mourinho amesema anataka  mlinda mlango Petr Cech  aendelee kubaki Stanford Bridge licha ya  kumpanga  Thibaut Courtois katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya England ambapo Chelsea ilishinda magoli 3 kwa 1 dhidi ya Barnley  jana usiku.
Courtos mwenye umri wa miaka 22  amerejea Chelsea baada ya kucheza kwa mkopo  wa miaka mitatu ndani ya mabingwa wa ligi kuu ya Hispania Atletico Madrid na ujio wake umefanya amweke benchi Cech ambaye alikuwa chaguo la kwanza.
Cech  mwenye umri wa miaka 32 tangu awasili Chelsea mwaka 2004 alikuwa chaguo la kwanza na ujio wa Courtois umemfanya  awe kwenye wakati mgumu kiasi cha kufikiria kuondoka lakini Mourinho amesistiza raia huyo wa jamhuri ya Cech bado anamhitaji.
Mourinho amesema tayari ameshaongea na Cech juu ya hali halisi ilivyo hivi sasa klabuni hapo  licha ya mlinda mlango huyo kutofurahia amemweleza kwamba anapaswa kukuliana nayo kwakuwa soka ndivyo lilivyo.

   Thibaut Courtois chaguo la kwanza la  sasa kwa Jose Mourinho.


                                       
                          Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment