Kiungo wa
zamani wa Manchester United Paul Scholes amesema timu hiyo inahitaji kufanyiwa
mabadiliko makubwa kama inataka kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu
ujao.
Akizungumza
baada ya Manchester United kufungwa magoli 2 kwa 1 kwenye mchezo wake wa kwanza
wa ligi kuu ya England hapo jana dhidi ya Swansea City Scholes amesema ipo haja ya kocha mkuu Lous Van Gaan
kukiimarisha zaidi kikosi chake.
Mkongwe huyo
ambaye aliichezea United kwa mafaikio makubwa enzi zake amesema baada ya
kuondoka kwa Nemanja Vidic,Patrice Evra
na Rio Ferdinand Van Gaal alipaswa kusajili wachezaji wazoefu wa nafasi hizo na sio kama
alivyofanya.
Scholes amesema wachezaji Tony Kroon
aliyejiunga na Real Madrid akitokea Bayern Munich na Cesc Fabrigas aliyejiunga
na Chelsea akitokea Barcelona walikuwa sahihi kwa Manchester United.
Kauli ya
nyota huyo liyeichezea United michezo 700 inamaanisha kama kocha Louis Van Gaal
hatotumia vyema muda uliobaki wa usajili barani Ulaya kwakununua wachezaji
atakuwa na wakati mgumu kufuzu klabu bingwa Ulaya msimu ujao.
MATOKEO YA MICHEZO YA JANA BPL HAYA HAPA.
LEO TAREHE 17.08.2014.
Liverpool vs Southampton.saa 15:30
Newcastle United vs Manchester City saa 18:00
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment