Pages

Ads 468x60px

Friday, August 29, 2014

QPR YATAKA KUMBAKISHA LOIC REMY LOFTUS ROAD.



                                      Loic Remy.

Klabu ya soka ya Queens Park Rangers imeahidi kumpa mkataba mpya mshambuliaji wake Loic Remy ambaye hivi karibuni alishindwa kufaulu vipimo vya afya kujiunga na  timu ya Liverpool.
Remy mwenye umri wa miaka 27 kwasasa yupo kwenye mazungumzo  ya kupatiwa mkataba mpya lakini jambo hilo linatarajiwa kufanyika mara baada ya dirisha la usajili barani Ulaya  kufungwa siku ya jumatatu ijayo.
Kocha wa QPR Harry Redknapp amemwanzisha mshambuliaji huyo raia wa Ufaransa katika michezo miwili ya awali ya ligi kuu ya England ambapo  timu hiyo ilipoteza yote kwakufungwa na Hull City na Tottenham hot spurs.
Licha ya vilabu kadhaa kuendelea kuonyesha nia ya kumsajili nyota huyo ikiwemo Newcastle United  kocha Harry Redknapp amebainisha kuwa  hadi kufikia septemba mosi mchezaji huyo atakuwa amesaini mkataba mpya.

                                     Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment