Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 7, 2014

PSG YANAWA MIKONO,USAJILI WA DI MARIA.





                   Rais wa timu ya PSG Nasser Al-Khelaifi.

Mabingwa wa ligi kuu ya Ufaransa PSG wamejiondoa katika mbio za kuwania sahihi ya nyota wa Real Madrid ya Hispania Angel Di Maria ambaye kwa majuma kadhaa wamekuwa kwenye mazungumzo.

Rais wa timu hiyo Nasser Al-Khelaifi ametangaza rasmi kujiondoa katika vita ya kutaka kumsajili nyota huyo raia wa Argentina kwakile alichoeleza anauzwa bei kubwa na hawawezi kumtwaa.

Al-Khelaifi amebainisha kuwa baada ya kufanya mazungumzo na rais wa Real Madrid Florentino Perez wameshindwa kufikia muafaka kuuziana mchezaji huyo kutokana na dau wanalolitaka kuwa kubwa na hawana budi kusitisha majadiliano hayo.

Tayari PSG chini ya kocha wake mkuu Laurent Blanc imesha msajili mlinzi wa kibrazil David Luiz kutoka Chelsea kwakiasi cha Euro milioni 50 msimu huu na pia imemsajili Serge Aurier kwa mkopo kutoka Toulouse.

                   Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment