Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 14, 2014

TIGER WOOD KUIKOSA MICHUANO YA RYDER.




                                                               Tiger Wood.

Mchezaji wa mchezo wa gofu Tiger Wood ametangaza kutoshiriki mashindano ya kombe la Ryder ambayo yanatarajiwa kuanza mwezi ujao nchini Scotland.
Tiger mwenye umri wa miaka 38 anayechezea timu ya taifa ya Marekani amekuwa akisumbuliwa mara kwa mara na maumivu ya mgongo ambayo yalimsababishia kufanyiwa upasuaji mapema mwezi wa tatu mwaka huu.
Ameongeza kuwa anasikitishwa kushindwa kujiunga na kikosi hicho kwani alipanga kutetea nchi yake katika mshindano hayo ya Ryder ambayo yanataraji kuanza tarehe 23 hadi 28 mwezi ujao nchini Scotland.
Hata hivyo nyota huyo wa mchezo wa gofu amemuomba radhi kocha wa timu ya taifa ya mchezo huo Tom Watson kuwa hatoweza kushiriki mashindano hayo kutokana na wataalamu wake wa afya kumtaka apumzike kwanza ili aweze kupona vizuri.
                          Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment