Pages

Ads 468x60px

Monday, August 25, 2014

SAFARI YA DI MARIA YAIVA, KUTUA LEO OLD TRAFORD KUKAMILISHA MAZUNGUMZO.



                                      Angel di maria.

Uongozi wa Manchester United umefikia makubaliano na Real Madrid juu ya kumsajili mshambuliaji Angel di Maria kwa ada ya paundi milioni sitni na tatu nukta tisa uliovunja rekodi ya uhamisho nchini England.
Kwamujibu wa kituo cha Sky Sport Di Maria mwenye umri wa miaka 26 raia wa Argentina anatarajiwa kusafiri leo kuelekea jijini Manchester  kukamilisha taratibu za kujiunga na mabingwa hao mara 20 wa ligi kuu ya England huku ikielezwa upo uwezekano mkubwa wa kupewa jezi namba 7 iliyowahi kuvaliwa na wachezaji mbalimbali maarufu walioichezea timu hiyo kama C.Ronaldo,David Bekham na wengineo.
Kocha mkuu wa Real Madrid Carlo Ancelotti jana jumapili amethibitisha kuwa Di Maria aliwasili kwenye mazoezi ya timu hiyo kwaajili ya kuwaaga wachezaji wenzake  pamoja na wafanyakazi wengine wa mabingwa hao wa Ulaya kwa vilabu.
Pia kiungo wa Real Madrid Xabi Alonzo amemtakia mafanikio mema dimaria kwakuandika kupitia ukurasa wake wa twiter kukumwambia daima hatosahaulika Santiago Bernabeu  kutokana na mchango mkubwa alioutoa akiwa klabuni hapo.

Kwa upande mwengine kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti amesema  mchezaji Sami Khedira hatoondoka klabuni hapo msimu huu na tayari uongozi wa timu hiyo umemhakikishia  kwamba atabaki.


Angel di Maria.

 

REKODI YA USAJILI KWA KLABU ZA UINGEREZA.

2011 Fernando Torres £50m Liverpool to Chelsea
2013 Mesut Ozil £42.4m Real Madrid to Arsenal
2011 Sergio Aguero £38m Atletico Madrid to Manchester City
2014 Juan Mata £37.1m Chelsea to Manchester United
2011 Andy Carroll £35m Newcastle to Liverpool
2014 Alexis Sanchez £35m Barcelona to Arsenal


                                      Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment