Pages

Ads 468x60px

Friday, August 8, 2014

BREKING NEWSSS,DROGBA ASTAAFU KUICHEZEA TIMU YA TAIFA.

                                                                             Didier drogba.
Mhambuliaji mkongwe wa timuu ya taifa ya Ivory Coast na klabu ya Chelsea Didier Drogba atangaza kustaafu kuitumikia timu yake ya taifa baada ya kuitumikia kwa miaka 12.

Drogba mwenye umri wa miaka 36 hivi asasa amefunga magoli 65 katika michezo 104 aliyoichezea timu ya taifa ya Ivory Coast na fainali za kombe la dunia mwaka huu zilikuwa za mwisho kwenye historia ya maisha yake ya soka.
Akizungumza baada ya uamuzi wake wa kustaafu Drogba ameandika kwenye ukurasa wake wa Twita kuwa anajisikia huzuni sana hasa ikizingatiwa amelitumikia taifa lake kwa miaka 12.
Drogba ambaye msimu huu amesajiliwa kwa mara nyingine na Chelsea  na kusaini mkataba wa mwaka mmoja amesema anajivunia kuwa nahodha wa timu ya taifa kwa miaka minane na kwa muda huo ameshiriki kombe la dunia mara 3,kuiwezesha nchi hiyo kufuzu fainali za AFCON mara 2.
Mchezo wa kwanza wa droba kuichezea timu ya taifa ya Ivory Coast ulikuwa dhidi ya Afrika ya kusini September mwaka 2002.
Drogba  kwa mara ya kwanza kucheza kombe la dunia ilikuwa mwaka 2006 na kufunga goli  kwenye pambano  la ufunguzi dhidi ya Argentina ambapo timu yake ilifungwa magoli 2 kwa 1.
Drogba pia akacheza tena fainali za kombe la dunia mwaka 2010 lakini hakufunga goli lolote katika michezo mitatu aliyocheza na hata katika fainali za mwaka huu Tembo hao wa Ivory Coast wameshindwa kufurukuta baada ya kutolewa hatua ya makundi.



                               Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment