Pages

Ads 468x60px

Friday, August 15, 2014

KUN AGUERO KUSALIA MANCHESTER CITY HADI 2019.




                                                                   Sergio Aguero.

Mshambuliaji wa mabingwa wa ligi kuu ya England Manchester City Sergio Aguero amerefusha mkataba wake kwakuongeza miaka mingine mitano ya kuendelea kuichezea timu hiyo yenye maskani yake jijini Manchester.
Aguero mwenye umri wa miaka 26 mkataba wake mpya aliyeuongeza utamfanya aendelee kuitumikia klabu hiyo hadi mwaka 2019  tangu ajiunge nayo mwaka 2011 akitokea kwa mabingwa wa La Liga Atletico Madrid.

                     Sergio Aguero City iliposhinda taji la kwanza la ligi kuu ya England.

Raia huyo wa Argentina tangu ajiunge na City  amefunga magoli 75 katika michezo 122 aliyocheza  na kuongeza kwake mkataba  mpya  kumefuta uvumi uliyoanza kuzagaa kuwa nyota huyo anampango wa kuihama timu hiyo.
Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo Aguero amesema najisikia furaha kuitumikia timu pekee yenye ushirikiano mkubwa kuanzia mashabiki,wachezaji na viongozi na hilo ndilo lililofanya wawe na mafanikio makubwa.

                                   Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment