Pages

Ads 468x60px

Monday, August 11, 2014

MAN CITY YAMTWAA RASMI MANGALA KUTOKA FC PORTO.





                                  Eliaquim Mangala.
Mabingwa  wa ligi kuu ya England timu ya Manchester city wametangaza rasmi kumsajili mlinzi wa kifaransa Eliaquim Mangala kutoka Fc Porto ya Ureno kwa uhamisho wa Euro milioni 40.
Mangala ambaye alikamilisha vipimo vya Afya mwezi july  mara baada ya kukamilisha uhamisho huo amesema anajisikia furaha kuhamia Manchester City kwakuwa ni mmmoja ya vilabu vikubwa barani Ulaya na anamatumaini ya kuendeleza kipaji chake.
Mangala amesema lengo lake kuu la kujiunga na Manchester City ni kutwaa mataji mbalimbali na huku akiisifu ligi kuu ya England ni kati ya ligi bora duniani na yenye ushindani mkubwa sana.

Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 23 amesema anajisikia furaha kucheza na wafaransa wenzake ndani ya Man City,Bacaray Sagna,Gael Clich na Samir Nasri kwakuwa wamekuwa wakicheza wote kwenye timu ya taifa.
Mangala amekuwa mchezaji wa 6 kujiunga na Manchester City msimu huu wa usajili akiungana na nyota wengine watano ambao ni Sagna, Fernando, Willy Caballero, Frank Lampard na Bruno Zuculini.
                                          Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment