Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 28, 2014

ETO'O ASTAAFU KUICHEZEA TIMU YAKE YA TAIFA YA CAMEROON.



                                            Samuel Eto'o.

Mshambuliaji mpya wa Everton raia wa Cameroon Samuel Eto’o ametangaza kustaafu kuichezea timu yake ya taifa tangu aanze kuitumikia nchi yake mwaka  1995 ambapo Cameroon ilifungwa magoli 5 kwa 0 na Costa Rica.
Eto’o mwenye umri wa miaka 33 amestaafu akiwa anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji wa muda wote kwa timu yake ya taifa baada ya kupachika magoli 56 licha ya kutofunga goli lolote kwenye fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Mshambuliaji huyo katika historia yake  amevichezea vilabu mbalimbali barani Ulaya kama Real Madrid,Marlloca, Fc Barcelona,Inter Milan, Anzhi Makhachkala,Chelsea,na sasa  anaichezea Everton akijiunga kwa uhamisho huru nakupewa mkataba wa miaka miwili akitokea Chelsea.
Akizungumza uamuzi wake wa kustaafu Eto’o ambaye ni kati ya wachezaji wa kiafrika waliowahi kukumbwa na maswahibu ya kubaguliwa kutokana na rangi yake  barani Ulaya amewashukuru waafrika wote hususani masahabiki wake kwa kuumuunga mkono na kumpenda.
Uamuzi wake ametangaza kupitia matandao wa kijamii wa Instagram.

Michezo ya kimataifa aliyocheza tangu 1997-2014 kwenye timu ya taifa ya Cameroon.

Year
Apps
Goals
1997
3
0
1998
5
0
1999
1
0
2000
9
5
2001
9
2
2002
13
5
2003
7
2
2004
9
4
2005
6
1
2006
5
5
2007
3
1
2008
11
11
2009
8
5
2010
12
8
2011
9
4
2012
2
0
2013
4
2
2014
2
1
Total
117
56

                                                 Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment