Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 27, 2014

GHANA YAUNGANA NA TANZANIA KUOMBA KUANDAA AFCON 2017.



                         Mashabiki wa timu ya taifa ya Ghana.

Nchi ya Ghana imetuma ombi la kuandaa fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2017  baada ya Libya kujitoa juma lililopita  kuwa mwenyeji kutokana na hali ya kisiasa ilivyo hivi sasa  kwenye taifa hilo la kaskazini mwa Afrika.
Ombi la Ghana kutaka kuandaa fainali hizo linatokana na tangazo lililotolewa jumanne  iliyopita na shirikisho la soka barani Afrika  CAF na mwisho wa kupokea maombi hayo ni September 30 mwaka huu.
Uongozi wa  shirikisho la mpira nchini Ghana umethibitisha kupewa baraka zote na serikali yao kutuma ombi hilo  kupitia kwa mwaklishi wa rais wa taifa hilo John Dramani  na kusema wanamatumaini makubwa ya kupewa heshima ya kuandaa michuano hiyo.
Ghana inaungana na  mataifa kadhaa yaliyomba nafasi hiyo ya kuwa mwenyeji wa fainali hizo za mwaka 2017,nchi nyingine  ni Kenya,Tanzania na Rwanda  ambazo tayari zimeshawasilisha maombi yao CAF.
                                    Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment