Pages

Ads 468x60px

Monday, August 11, 2014

ZLATAN:SINAMPANGO WA KURUDI JUVENTUS.




                                                        Zlatan Ibrahimovic.

Nyota wa mabingwa wa ligi kuu ya Ufaransa Zlatan Ibrahimovic amekanusha habari zilizozagaa zakusema anampango wa kurudi katika timu ya Juventus ambao ni mabingwa wa ligi kuu ya Italia Serie A.
Zlatan ambaye ni raia wa Swiden amesema hamjui mtu aliyejitambulisha kwa jina la Stefan Hansson aliyekaririwa na vyombo vya habari akisema kwamba yeye anampango wa kurudi Italia kuichezea timu ya Juventus.
Hansson hivi karibuni alikaririwa na baaadhi ya vyombo vya habari barani Ulaya akisema anaurafiki wa karibu na nyota huyo tangu alipokuwa akiichezea Malmo na kwamba anauhakika wa Zlatan kurudi Italia lakini nyota huyo amekana kumtambua.
Ibrahimovic ambaye alifunga magoli mawili mwishoni mwa juma lililoisha jana  dhidi ya Reims ambapo pambano hilo lilimalizika kwa sare ya magoli 2 kwa 2 mkataba wake na PSG unamalizika  mwezi wa sita mwaka 2016.

                                Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment