Pages

Ads 468x60px

Sunday, August 17, 2014

MANOLAS KUFANYIWA VIPIMO VYA AFYA ARSENAL.




                                                                Kostas Manolas
Mlinzi wa klabu ya Olympiakos ya Ugiriki Kostas Manolas  anajiandaa kwenda kufanyiwa vipimo vya afya tayari kwa kujiunga na timu ya Arsenal inayoshiriki ligi kuu ya England kuziba nafasi ya Thomas Vermaelen aliyejiunga na Fc Barcelona.
Imeripotiwa kuwa Arsenal ilianza mazungumzo na Olympiakos mapema mwezi huu na pande hizo mbili zinaelezwa kufikia makubaliano ya kuuziana mchezaji huyo kwa uhamisho wa Euro milioni 10.
Hivi karibuni kocha wa Arsenal mfaransa Arsene Wenger alikaririwa akisema  atafanya usajili wa nafasi ya ulinzi wakati licha ya kumsajili Calum Chambers kwa ada ya Euro milioni ishirini.
Arsenal ambayo jana ilipata ushindi wa magoli 2 kwa1 ikiwa nyumbani dhidi ya Crystal Palace  pamoja na kuwa kwenye nafasi nzuri ya kumsajili Kostas Manolas  nayo timu ya Juventus ya Italia imeonyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo.



                           Mkule.blogsports.com

No comments:

Post a Comment