Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 7, 2014

REINA AFAULU VIPIMO LEO KUSAINI MKATABA NA MABINGWA WA BUNDESLIGA




                                                                    Pepe Reina.

Mlindamlango Pepe Reina leo ijumaa anataraji kusainikataba na maabingwa wa ligi kuu ya ujerumani Bundesiliga Fc Bayern Munich baada ya kufaulu vipimo alivyofanyiwa jana Alhamisi.
Tayari uongozi wa Bavarian umethibitisha kupitia ukurasa wao wa Twiter kuwa Reina atasaini mkataba huo leo ijumaa  baada ya klabu yake ya Liverpool kufikia makubaliano na kikosi hicho kinachofundishwa na kocha Pep Guadiola.
Reina alijunga na Liverpool mwaka 2005 mwezi julai na kushinda kombe la FA ,kombe la ligi kwa  muda wote akiwa na vijogoo hao wa Anfield.
Pamoja na kucheza kwa mkopo msimu uliopita kwenye klabu ya Napoli ya Italia Reina amepoteza nafasi ya kuwa golikipa namba moja wa Liverpool kutokana na mlinda mlango wa sasa Simon Mignolet kuaminiwa zaidi na kocha mkuu Brendan Rogers.
Akiwa Beryen munich Reina anatarajiwa kuwa mlinda mlango namba mbili nyuma ya Manuel Neuer pale Allianz Arena mjini Munich
                             Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment