Mlindamlango wa El merekh Salim Omar Magoola, mwenye umri wa miaka 21 aliyeibuka shujaa kwa kuokoa mikwaju miwili ya penalti sambamba na kufunga penalti ya mwisho na kuitoa kimasomaso timu yake na kutinga fainali ya Kagame 2014 mjini Kigali Rwanda.
Timu za El
merekh ya Sudani na APR ya Rwanda zimefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya m
ichuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati maarufu kama kagame baada ya
kushinda michezo yao ya nusufainali hapo jana.
Wakati El
merekh ikifunga KCCA ya Uganda kwenye nusu fainali ya kwanza iliyochezwa uwanja
wa Amahoro mjini Kigali Rwanda kwa changamoto ya mikwaju ya penalty 3 kwa 0, APR yenyewe nayo imetinga
hatua hiyo kwakuifunga ndugu zao Polisi Rwanga
kwa mikwaju ya penalt 4 kwa 2.
APR na
Polisi zilifikia hatua ya kupigiana matuta baada ya kutoka suluhu katika dakika
120 ndipo waliolazimika kupigiana changamoto ya mikwaju ya penalty wakati El
merekh yenyewe pia iliiondosha KCCA ya Uganda kutokana na kufungana magoli 2
kwa 2 ndani ya dkk 120.
Kwamatokeo hayo
hatua ya fainali itakayofanyika kesho mjini Kigali Rwanda itakuwa baina ya El merekh ya Sudani na APR
ya Rwanda pambano litakalochezwa kunako dimba la Amahoro.
Mbali na
pambano hilo la fainali mchezo mwengine utakuwa ni wa kusaka mshindi wa tatu baina
ya KCCA ya Uganda na Polisi ya Rwanda michezo yote ikichezwa kunako dimba la
Amahoro.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment