Na Boniface
Wambura, DAR ES SALAAM.
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limezuia mechi zake kuchezwa Guinea, Liberia na Sierra Leone kutokana na kuripotiwa kuwepo kwa wagonjwa wengi wa Ebola katika nchi hizo.
Ikiwa ni njia mojawapo ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya ugonjwa huo kupitia mkusanyiko wa watu, CAF imevitaka vyama vya mpira wa miguu vya nchi hizo kuchagua viwanja vingine huru kwa ajili ya timu zao zinazoshiriki michuano yake kwa kipindi hiki hadi katikati ya mwezi ujao.

Pia kutokana na mapendekezo ya Shirika la
Afya Duniani (WHO), CAF imesema kwa nchi zenye virusi vya Ebola ni muhimu kwa
vyama vyake vya mpira wa miguu kuufanyia vipimo vya afya msafara wa timu zao
ili kuhakikisha wenye virusi vya ugonjwa huo hawasafiri.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment