Pages

Ads 468x60px

Sunday, August 17, 2014

HEPAUTWA CUP 2014 YAANZA MJINI IRINGA.





                                    Waamuzi wanaosimamia michuano ya Hepautwa cup 2014.

Baada ya pazia la michuano ya Hepautwa cup 2014 kufunguliwa hapo jana katika uwanja wa  kumbukumbu ya Samora mjini Iringa mashindano hayo yanatarji kuendelea tena leo kwa mchezo mmoja.
Kwamujibu wa ratiba hiyo timu ya Mlandege fc inataraji kuikabili Ilala fc kwenye uwanja huo wa Samora hii ikiwa ni hatua ya awali ya mtoano ambapo timu inayoshinda ndiyo inayosonga mbele na inayoshindwa inatoka.
Akizungumza katika mchezo wa ufunguzi hapo jana mdhamini wa mashindano hayo Ndg.Nuru Hepautwa alisema lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kutoa fursa kwa vijana wa mjini Iringa na mkoa wa Iringa kwaujumla kucheza soka.
Hepautwa aliwataka wachezaji wote kucheza kwa nidhamu kwakuwa soka na ajira nzuri hivi sasa huku akiahidi kutoa ushirikiano  kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mashindano hayo.

Katika mchezo wa ufunguzi Makorongoni fc iliibuka na ushindi wa magoli 6 kwa 0 dhidi ya Gangilonga.

        Mdhamini wa mashindano ya Hepautwa cup 2014,Nuru Hepautwa akikagua timu hapo jana kwenye uwanja wa Samora.

Ifutayo ni ratiba ya michuano hiyo hatua ya mtoano michezo yote ikichezwa katika uwanja wa kumbukumbu ya samora.
17/08/2014.
Mlandege 1 vs 0 Ilala fc.
18/08/2014.
Isakalilo 5 vs 4 ruaha.
19/08/2014.
Kitwiru vs kihesa.
20/08/2014.
Mwangata vs mtwivila city.
21/08/2014.
Kitanzini vs mkwawa.
22/08/2014.
Mivinjeni vs mshindo.

Timu ya kwakilosa itaungana na timu zilizofuzu hatua ya mtoano kwamujibu wa kanuni za mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment