Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 7, 2014

DONOVAN KUSTAAF SOKA BAADA YA KUMALIZIKA KWA LIGI KUU YA MAREKANI MSIMU HUU.




                                                                    London Donovan.


Mshambuliaji wa klabu ya LA Galaxy ya nchini Marekani London Donovan ametangaza kustaafu soka mara baada ya kumalizika kwa msimu mpya wa ligi kuu ya MLS (Major League Soccer).
Akiwa  na umri wa maiak 32 Donovan ameshafunga magoli 57 kwenye michezo 156  kwenye timu ya taifa ya Marekani na ndiye mfungaji wa muda wote wa timu  hiyo.
Akizungumza na waan dishi wa habari nchini Marekani Donovan amesema  anajisikia furaha kucheza kwenye ligi  kuu ya nchi hiyo  nakuwashukuru wote waliomuunga mkono katika kazi yake ya kucheza soka.
Pia nyota huyo amewahi kucheza michezo 22 na kufunga magoli 2 akiwa kwa mkopo katika timu ya Everton ya nchini England  mwaka 2010 na 2012 lakini pia amewahi kuzichezea timu za Bayer Leverkusen na Bayern Munich.
Aidha Donovani ambaye amecheza fainali za mwisho kwake za kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika ya kusini ameahidi kuendelea kuwa  karibu na watu mbalimbali waliyopo kwenye mchezo anaoupenda zaidi.
Donovan ambae hakuwepo kwenye kikosi cha marekani kilichoshiriki fainali za mwaka huu za kombe la dunia huko Brazil chini ya kocha mkuu Jurgen Klinsmann atahitimisha maisha yake ya soka mwezi wa 10 mwaka huu baada ya kumalizika kwa msimu wa ligi ya marekani  MSL. 


                                       Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment