Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 20, 2014

ROJO AMWAGA WINO WA KUITUMIKIA MANCHESTER UNITED KWA MIAKA MITANO.

                                                                           Marcos Rojo

Klabu ya manchester United imethibitisha kupitia tovuti yake kukamilisha usajili wa mlinzi Marcos Rojo kutoka Sporting Lisbon ya Ureno kwa mkataba wa miaka mitano uliowagharimu kiasi cha paundi milioni 16 nakupewa jezi namba 5 iliyokuwa ikivaliwa na Rio Ferdnand aliyekiujga na QPR.

Rojo mwenye umri wa miaka 24 ambaye alijiunga na Sporting Lisbon akitokea Spartak Moscow alianzia soka lake kwenye klabu ya Estudiantes de la Plata ya kwao Argentina na tangu aanze kuichezea timu yake ya taifa miaka mitatu iliyopita amecheza michezo 28.
Amesema kuvaa jezi ya United ni heshima kubwa katika maisha yake ya soka kwakuwa ni mionongoni mwa vilabu vikubwa na bora zaidi duniani ikiwa chini ya kocha aliyemwita mwenye uzoefu mkubwa Louis van Gaal .
 Pamoja na kuahidi kuichezea United kwa moyo wake wote Rojo amesema atahakikisha anaisaidia timu hiyo kutwaa mataji makubwa kwamuda wote atakaokuwa anaitumikia.
 Naye kocha Louis van Gaal amesema Rojo ni mlinzi mzuri aliyebarikiwa kipaji cha hali ya juu  hivyo ujio wake ndani ya United ni zawadi kubwa.
                           Marcos Rojo akionesha jezi yake no,5 atakayokuwa akivaa ndani ya Man U.

 
Marcos Rojo
   
                                                         Marcos Rojo akiwa kwenye pozi.

                              Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment