Uchaguzi wa
kupata viongozi wapya wa timu ya soka ya Lipuli ya mkoani Iringa unataraji
kufanyika tarehe 28 ya mwezi 9 mwaka huu ambapo nafasi mbalimbali zinawaniwa
ikiwemo nafasi ya Uenyekiti ukatibu pamoja na wajumbe wa kamati ya utendaji.
Kwamujibu wa
mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi huo Jackson Abraham Chaula Amesema muda wa kuchukua na kurudisha fomu za kugombea
zitaanza kutolewa kesho tarehe 24/08/2014 kwa nafasi zote hadi tarehe 28 ya
mwezi huu wa nane mwaka huu wa 2014.
Kwamujibu wa
mwenyekiti wa kamati hiyo 29/08 hadi 30/08 mwaka huu kitafanyika kikao cha
mchujo wa awali wa wagombea zoezi litakalosimamiwa na kamati hiyo ya uchaguzi.
31/08/2014 ni kuchapisha
na kubandika kwenye mbao za matangazo orodha ya awali ya wagombea na tarehe 01 ya mwezi wa 9 ni kipindi cha kuweka
pingamizi kwa wagombea zoezi litakalenda hadi 04/09/2014.
Tarehe 7/09
hadi 8/09 2014 kupitia pingamizi zote na
kufanyia usaili wagombea wa uchaguzi huo na tarehe 7/09 hadi 8/09 2014 kipindi
cha kupokea ,kusikiliza na kutoa majibu ya masuala ya kimaadili.
Pamoja na
taratibu zingine zitakzofuata baada ya hapo kabla ya uchaguzi huo utakaofanyika
September 28 mwaka huu sifa za muombaji
ni
1.Kuwa raia
wa Tanzania.
2.Awe na
sifa zinazohitajika kwa nafasi anayoiomba na awe amelipa ada ya uanachama
kikamilifu tangu aanze uanachama.
3.Awe na
kiwango cha chini cha elimu ya kuanzia kudato cha nne yenye uthibitisho kutoka baraza
la mitihani la taifa.
4.Asiwe aliyewahi kutiwa hatiani kwa kosa la
jinai kwa kutuhumiwa kifungo.
5.Awe na
umri angalau kuanzia miaka 25.
6.Awe
ametimiza angalau miezi 6 ya uanachama.
7.Asiwe
mwamuzi wa soka anayefanya shughuli za uamuzi kwa kipindi hiki.
Gharama za
fomu.
Mwenyekiti ,makamu
mwenyekiti,.Laki 1
Katibu na
katibu msaidizi …Laki 1.
Mweka hazina
na mweka hazina msaidizi ...Elfu 50,
Wajumbe wa5
wa kamati ya utendaji ..Elfu 50
Mwekahazina msaidizi……Elfu
50
Fomu zinapatikana
VETA Iringa onana na Ramadhani Mahano.
Mshindo kwa…..Fundi
Rajabu.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment