Gerardo Martino kocha mpya wa timu ya taifa ya Argentina.
Shirikisho la soka nchini Argentina
limemtangaza kocha wa zamani wa Fc Barcelona Gerardo Martino kuwa kocha wa timu
ya ya taifa kuchukua nafasi ya Alejandro Sabella aliyeachia ngazi mara baada ya
kumalizika fainali za kombe la dunia ambapo Argentina ilifungwa goli 1 kwa 0 na
Ujerumani.
Martino mwenye umri wa miaka 51
aliondoka Barcelona mwishoni mwa msimu uliopita
baada ya kuifundisha timu hiyo kwa mwaka mmoja na kushindwa kutwaa taji hata mmoja kwa mara
ya kwanza tangu msimu wa 2007-2008.
Martino alipewa kibarua cha
kuifundisha Fc Barcelona mwezi july
mwaka 2013 kuchukua nafasi ya marehemu Tito Vilanova nakusaini mkataba wa miaka
miwili lakini kutokana na kushindwa kupata mafanikio alifukuzwa kazi na nafasi
yake ikachukuliwa na Luis Enrique.
Martino aliwahi kuwa kocha wa timu
ya taifa ya Paraguay kati ya mwaka 2006 na 2011 na kuifikisha robo fainali
katika fainali za kombe kla dunia mwaka 2010.
Martino anataraji
kutambulisha kesho Alhamisi mbele ya
vyombo vya habari tayari kuwa kocha mkuu wa Argentina.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment