Samir Nasri.
Nasri
amesema kuwa amekuwa akiwaza kustaafu
kuitumikia timu yake ya taifa tangu mwaka 2012 mara baada ya fainali za kombe
la mataifa ya Ulaya nasasa anathibitisha
rasmi kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Ufaransa.
Nasri
amesema hadhani kama atafikiria kubadili uamuzi wake maka timu ya taifa
itaendelea kuwa chini ya kocha Didier Deschamps.
Nasri
mwenye
umri wa miaka 27 amesema amesikia taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa
baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa walikuwa wanalalamika kwanini
hakujumuishwa na kocha kwenye kikosi cha Ufaransa kilichokuwepo Brazil
hali inayomaanisha hata wachezaji wenzake wapo katika makundi.
Nasri
amesema kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa alikaririwa na vyombo vya habari
akisema hakumuita katika timu ya taifa
kutokana kumuona hana furaha nakuongeza kwamba ni mchezaji gani ambaye hufurahia kukaa
benchi.
Nasri ambaye aliadhidiwa kutocheza michezo mitatu bada ya michuano ya Euro 2012 kutokana na kutoa lugha chafu kwa waandishi wa habari ameongeza kuwa familia yake haijisikii furaha na kitendo cha yeye kuanchwa kwenye kikosi cha taifa hivyo uamuzi wake wa kustaafu utawapunguzia maumivu.
Katika
timu ya taifa Nasri amefunga magoli 5 katika michezo 41 aliyocheza.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment