Pages

Ads 468x60px

Friday, August 22, 2014

SUPER MARIO BALOTELLI KUWASILI MCHANA HUU LIVERPOOL KUFANYIWA VIPIMO.



                        Super Mario Balotelli akiwa na baybe wake.

Wakati mshambuliaji Mario Balotelli akitaraji kuwasili leo Uingereza kufanyiwa vipimo vya Afya mchana huu  katika timu ya Liverpool hata akifaulu vipimo hivyo  hatopangwa kwenye mchezo wa jumatatu ambapo Liverpool  itakuwa ikicheza na Manchester City.
Liverpool ambayo ipo tayari kumpatia Balotelli mkataba wa miaka mitano na mshahara wa paundi laki moja na elfu ishirini kwa juma imebainisha kuwa watahitaji kutambua utayari wa mchezaji huyo pamoja na suala la nidhamu kabla ya kupangwa kuchezwa.
Tayari Liverpool imeshakubaliana na AC Milan juu ya kuuziana mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliyewahi kuichezea Manchester City kwa uhamisho wa paundi milioni 16 na wengi wanadhani kuwa endapo Balotelli atafaulu vipimo ataikabili timu yake ya zamani ya Manchester City.

                                      Samwel Eto'o.

Katika hatua nyingine Uongozi wa Liverpool upo tayari kumpa makataba wa mwaka mmoja mchezaji Samweli Eto’o ambaye amemaliza mkataba wake na Chelsea msimu uliopita ili kuiongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji.

                            Mkuleblogsport.com.

1 comment:

  1. Super Mario.......!
    Usajili wa kweli ila ndo ngumi mkononi......njoo utupe raha, Mario Balotelli mzee wa magazeti haishiwi vituko.
    Mwana wa Madunda

    ReplyDelete