Pages

Ads 468x60px

Tuesday, August 26, 2014

ATLETICO MADRID YAKATA RUFAA KUPINGA ADHABU ALIYOPEWA KOCHA WAO MKUU DIEGO SEMIONE.



Diego Semione aliyevaa suti hapo akimzungumza na kamisaa wa mchezo kwenye pambano dhidi ya Real madrid juma lililopita.

Uongozi wa mabingwa wa ligi kuu ya Hispania klabu ya Atletico Madrid umesema haujakubaliana na adhabu aliyopewa kocha wao mkuu Diego Semione  ya kufungiwa michezo 8 iliyotolewa na shirikisho la soka nchini humo baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu kwenye mchezo wa Spanish Super cup.
Rais wa klabu hiyo Enrique Cerezo amesistiza kwamba hawakubaliani na adhabu hiyo ambayo imetokana na kocha huyo kuvunja sheria uwanjani siku ya mchezo dhidi ya Real Madrid juma lilopita  kwenye uwanja wa Vicente Calderon.
Rais huyo amesema mara baada ya kuwasilisha rufaani yao ya kupinga adhabu hiyo  watasubiri majibu  lakini  akisistiza adhabu hiyo ni kubwa  kulikokosa alilolifanya kocha huyo raia wa Argentina.
Katika mchezo huo uliochezwa mwishoni mwa juma lilopita kocha huyo alikiuka sheria kwakuvuka eneo analotakiwa kukaa na pia alimsukuma kamisaa wa pambano hilo akishinikiza mchezaji wake aliyekuwa anatibiwa nje ya uwanja aruhusiwe kurudi uwanjani haraka.
                                    Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment