Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 14, 2014

HATMA YA RUFAANI YA SUAREZ KUJULIKANA LEO.




                                                Luis Suarez.

Mustakabali wa rufaani ya mshabuliaji  mpya wa Fc Barcelona Luis Suarez unataraji kujulikana leo ambapo mahakama ya masuala soka  duniani CAS mjini Uswis inasikiliza na kufanya maamuzi juu ya adhabu ya kufungiwa kwa mchezaji huyo miezi minne.
Suarez ambaye amepigwa marufuku kuingia  kwenye uwanja wowote wa soka hata wa timu yake ya Fc Barcelona sambamba na kutofanya mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake wa kikosi hicho  aliwasilisha rufani hiyo  kupinga adhabu  aliyopewa na shirikisho la soka duniani Fifa.
Katika mahakama hiyo ya CAS iliyopo mjini Lausanne Uswis Suarez atawakilishwa na wanasheria wake  akiwemo Daniel Cravo na mara baada ya rufani hiyo kusikilizwa taarifa rasmi itatolewa kwa vyombo vya habari.
Suarez kwasasa anatumikia adhabu ya kutocheza soka kwa miezi minne sambamba na kutoitumikia timu yake ya taifa ya Uruguay michezo minane kutokana na kumng’ata nyota wa Italia Giorgio Chiellini kwenye fainali za kombe la dunia mwaka huu zilizomalizika mwezi ulipita nchini Brazil.

                       Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment